24.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 25, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Rais Samia azindua Jengo Halmashauri ya Bumbuli, apongeza utunzaji mazingira Lushoto

Na Mwandishi Wetu, Lushoto

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amezindua jengo la Halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto mkoani Tanga ikiwa ni muendelezo wa ziara yake mkoani humo leo Februari 24,2025, huku akiwapongeza wananchi wa wilaya hiyo kwa utunzaji mzuri wa mazingira.

Akizungumza na wananchi  hao katika mkutano wilayani humo, amewataka wananchi hao kuendelea mazingira vizuri na kuwafundisha wengine juu ya utunzani mazingira.

“Kabla ya kuendelea na hotuba yangu, kwanza niwape wana Lushoto  maua yenu kwenye  utunzaji wa mazingira. Nataka niwaambie kweli ukiingia Lushoto hata uvutaji wa hewa unakuwa mwepesi zaidi. Kwa hivyo Lushoto naomba mfundishe wengine na muendelee kuweka mazingira yenu vizuri hongereni sana,”  amepongeza Rais Dk. Samia.

Kuhusu jengo hilo la Halmashauri, amesema madhumuni  ni kusogeza huduma karibu ambapo huduma zote zitakuwa zinapatikana ndani ya jengo hilo.

“Ndugu zangu jengo hili tumeliweka ili watumishi tunaowaleta  hukuwafanyie kazi humu ndani, mazingira mazuri ya kazi na nyinyi mpate huduma humu ndani, jambo zuri ni kwamba watumishi wote watakuwa humu ndani, hivyo wananchi wa Bumbuli mlitumie kupata huduma zenu,” amesema Dk. Rais Samia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
595,000SubscribersSubscribe

Latest Articles