31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Rais samia atumbua Wakurugenzi wanne, wa Geita awekwa kiporo

Na Mwandishi Wetu,Mtanzania Digital

RAIS Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Wakurugenzi 4 wa Halmashauri kwa matumizi mabaya ya Fedha za miradi ya maendeleo hususan ni zile za Ustawi na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Wakurugenzi hao ni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza, Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida mkoani Singida, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya mkoani Mbeya na Mbeya na Mkurugeniz wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa.

Akizungumza leo Ijumaa Februari 4, 2021 mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amesema halmashauri zote ambazo zimetuhuniwa kwa matumizi mabaya ya fedha za miradinakwamba uchunguzi umefanyika na kwa halmashauri ya Wilaya ya Geita uchunguzi unaendelea.

Rais Samia ameagiza uchunguzi uendelee katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo napo kuna tuhuma za namna hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles