30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Rais Samia atoboa siri ya kumteua Dk, Mpango

Erick Mugisha

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameeleza siri ya kumchagua Makamu wake Dk, Phillip Mpango leo machi 31, Ikulu chamwino.

Ameyasema hayo huku akishukuru bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kumpitisha Dk, Mpango kwa asilimia 100%.

Rais samia amesema kumteua Dk, mpango ni kutokana na uchapakazi wake, uzoefu wa kazi, Mcha mungu, pia ni mchumi mahiri

“Dk, Mpango nimemteua kwasababu hana mambo mengi na niliangalia majina ya watu wengi ndani na nje ya bunge, kabla ya kumteua na kuona atanifaa kwenda nae katika kazi.

Nimeona Dk, mpango atanifaa katika  maswala ya kiuchumi na udhibiti wa matumizi ya fedha za serikali”, alisema Rais Samia.

Pia Rais samia amaeogezea na kusema kazi iliyobaki ni shughuli ya mahusiano ya kifedha kati ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania pamoja na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na kazi hii amempatia Dk, Mpango kutekeleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles