25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia atajwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani 2022

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amechaguliwa na Jarida maarufu duniani la Times la nchini Marekani kuwa ni mmoja wa watu wa 100 wenye ushawishi mkubwa duniani kwa Mwaka 2022.

Rais Samia ambaye aliingia madarakani mwaka Machi, 2021 kufuatia kifo cha ghafla cha Rais John Pombe Magufuli amechaguliwa kwenye kundi la viongozi wenye ushawishi mkubwa kwa sasa duniani.

Wengine kwenye kundi hilo ni pamoja na Rais wa Marekani Joe Biden, Putin wa Urusi, Zelensky wa Ukraine, Xi Jinping wa China, Rais wa Umoja wa Ulaya, Ursula Von der Leyen, Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz, Letitia James ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa New York kutoka Chama cha Democratic pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Aby Ahmed.

Akimuelezea rais Samia baada ya uteuzi huo, Rais wa zamani wa Liberia Helen Sirleaf Johnson alisema toka achukue madaraka amefanya mabadiliko makubwa.

“Milango imefunguliwa kwa ajili ya majadiliano na maridhiano miongoni mwa mahasimu wa kisiasa, hatua zimepigwa katika kujenga upya imani ndani ya mfumo wa kidemokrasia, juhudi zimefanyika katika kuongeza uhuru wa habari na wanawake na wasichana hivi sasa wanaye mtu mpya mustakhbal wa maisha yao yaani mtu wa kuigwa(Role model)” alisema Rais hiyo zamani wa Liberia.

Amesema Septemba 21, mwaka jana Rais Samia alikuwa rais wa tano mwanamke kutoka Afrika kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kutoa hotuba nzito.

“Alisimama katika mahali(podium) ambapo mimi nilisimama miaka 15 iliyopita nikiwa Rais wa kwanza mwanamke kutoka Afrika kulihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa,” amesema na kuongeza:

“Rais Samia alisema hapa na mnukuu: ‘Nikiwa Rais wa kwanza mwanamke nchini mwangu, nabeba mzigo mzito wa matarajio ya kuleta usawa wa jinsia’ mwisho wa kumnukuu. Wakati anazungumza maneno haya mazito kabisa nilijikuta nikifikiri na kuwaza nguvu za mabega ya viongozi wanawake kubeba dhima hiyo na kwa umbali gani wataweza kutoa matokeo chanya,” amesema Sirleaf ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles