27 C
Dar es Salaam
Sunday, February 16, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Rais Samia apewa tano kwa mafanikio ya Sekta ya Utalii

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao, Steve Mengele maarufu Steve Nyerere, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mafanikio makubwa ya sekta ya utalii, ikiwemo kufikisha watalii milioni 5.3 na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa.

Steve ametoa pongezi hizo Januari 31, 2025 wakati wa hafla maalum ya kusherehekea mafanikio ya Tanzania katika sekta ya utalii iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kusema kuwa juhudi za serikali zimekuwa chachu ya ukuaji wa utalii wa ndani na nje.

“Tunatoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuamini na kuwekeza kwenye sekta ya utalii. Pia, tunaipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya uongozi wa Mheshimiwa Pindi Chana kwa ubunifu wao unaoendelea kuongeza pato la Taifa kupitia utalii,” amesema.

Aidha, amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Hassan Abbas, kwa juhudi zake katika kufanikisha ukuaji wa utalii wa ndani.

“Sisi kama Mama Ongea na Mwanao, tuko tayari kushirikiana na wizara kuhakikisha tunatangaza, kulinda na kudumisha utalii wa ndani kwa maendeleo ya Taifa,” ameongeza.

Steve amehitimisha kwa kuwataka wadau wote wa utalii kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kuhakikisha Tanzania inazidi kuwa kivutio kikuu cha watalii duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
594,000SubscribersSubscribe

Latest Articles