26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

Rais Samia aombwa kuingilia kati mahabusu wa kesi ya ugaidi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ameombwa kuingilia kati suala la mahabusu 117 ambao wamekuwa gerezani kwa miaka 10 katika magereza ya Ukonga, Segerea, Maweni, Kisonge, Morogoro, Mtwara, Tabora na Butimba mkoani Mwanza wakisubiri upelelezi kukamilika.

Baadhi ya ndugu hao.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Jumamosi Januari 28, 2023 jijini Dar es Salaam baadhi ya ndugu hao wameeleza kuwa ndugu zao hao wanashikiliwa tangu mwaka 2013 huku wengine wakishikiliwa tangu mwaka 2017.

Mmoja wa ndugu hao, Zubeda Rajab anesema wameamua kupaza sauti kumuomba Rais Samia awasaidie kwa kuwa ndiye alitamka kwamba katika Serikali yake mtu hatakamatwa kwa bila kuwa na ushahidi.

“Tumeamua kupaza sauti kwa sababu Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan amepata kutamka kwamba katika Serikali yake mtu hatakamatwa mpaka pale vyombo vya usalama vimepata ushahidi wa tuhuma dhidi yake. Pia amepata kutoa maelezo kuwa, katika Serikali yake raia waliowekwa magerezani kwa muda mrefu kwa hoja ya upande wa serikali kutafuta ushahidi wataachiwa huru,” amedai Zubeda.

Upande wake Khadija Mohamed amedai wamefikia hatua hiyo ya kumuomba Rais Samia aingilie kati jambo hilo baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila mafanikio huku wakizungushwa pindi wanapofika kwenye mamlaka husika ikiwamo Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

“Tuliamiani Serikali kupitia vyombo vyake vya kusimamia haki ndugu zetu wangetendewa haki. Tumekuwa tukienda katika mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam na Dodoma mara kwa mara bila mafanikio. Kwa mara ya mwisho ofisi hiyo ilituj majibu ya mdomo kuwa mpaka Julai 2022, ufumbuzi utapatikana ima kwa Serikali kupelet ushahidi mahakamni au mashauri hayo kufutwa, lakini mpaka leo ndugu zetu wameendelea kunyimwa haki,” amedai Khadija.

Upande wake, Abdulhamid Mkanda amedai kuwa, masheikh hao 117 ni kati masheikh zaidi ya 180 waliokuwa wanakabiliwa na tuhuma za ugaidi ambao walikamatwa na kusisitiza kuwa baadhi ya waliko gerezani tayari ni wazee.

“Mfano kuna mzee Suleman Ulatule Simbaambaye ana umri wa miaka 96 anashikiliwa gerezani miaka nane, zaidi ya hilo anashikiliwa gerezani yeye na familia yake ya watu sita na hakuna mtu wa kuwasaidia. Mfano mwingine kuna watoto waliokamatwa wakiwa na miaka 15 na 17, kwa madai kwamba walikusudia kuwakamata baba lakini hawakupatikana,”amedai Mkanda.

Itakumbukwa kwamba Mwaka 2021, Ofisi ya DPP iliwaacha huru baadh masheikh waliosota gerezani kwa zaidi ya miaka sita, wakikabiliwa na mashtaka ya ugaidi, baada kuwafutia kesi zilizokuwa zinawakabili kwa kukosekana kwa ushahidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,405FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles