22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia aipigia simu Twiga Stars

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Rais Samia Suluhu Hassan, amepiga simu kuipongeza timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars kutokana na kufurahishwa na kitendo cha wachezaji hao kutwaa ubingwa wa  COSAFA katika mashindano yaliyofanyika  nchini Afrika Kusini.

Rais Samia amepiga simu hiyo jana Oktoba 12,2021 wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyoandaliwa na Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kupitia kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Hassan Abbasi.

Katika hafla hiyo ya chakula cha usiku iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, pia timu ya wanawake ya U20, Tanzanite imepongezwa kwa kufanikiwa kutinga raundi ya tatu ya kufuzu Kombe la Dunia.

Twiga Stars

 Rais Samia amezitaka timu zote ziendelee kufanya vizuri ili kuitangaza Tanzania Kimataifa na kuahidi kukutana nazo uso kwa uso kutoa pongezi zake.

“Hongereni sana nimemuagiza katibu mkuu ale nanyi leo lakini nami nikija Dar, nitawaalika tuonane, hongereni sana kwa kazi nzuri,” amepongeza Rais.

Wageni waalikwa katika halfa hiyo  ikiwamo taasisi mbalimbali, zilitoa zawadi mbalimbali ikiwamo fedha kwa wachezaji wa timu hizo, huku  Dk. Abbasi  kwa niaba ya

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles