24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Rais Ramaphosa aahidi kukisafisha chama chake

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameahidi kukisafisha chama chake cha ANC wakati akijiandaa kuunda baraza jipya la mawaziri kufuatia ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa May 8.

Chama hicho kilishinda kwa asilimia 57 ya kura, ushindi mdogo kabisa katika kipindi cha miaka 25 ya chama hicho madarakani. Uitikiaji wa kiwango cha asilimia 65 ya wapigakura ilikuwa ishara nyingine ya kukata tamaa kwa wnanchi, kutokana na kashfa za ufisadi zilizokiandama chama cha ANC chini ya utawala wa Rais Jacob Zuma aliyejiuzulu mwaka jana.

Katika hotuba yake ya kwanza kwa wafuasi wa chama chake baada ya uchaguzi, Rais Ramaphosa alisema hatawateuwa katika baraza lake viongozi wanaofanya kazi kujaza mifuko yao binafsi.

Katika hotuba hiyo jana jioni, jioni alisema viongozi wa aina hiyo watake wasitake, atapigana kuutokomeza ufisadi, na amewataka viongozi wa chama chake kutofichiana siri za matendo maovu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles