33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Putin, Kim kukutana leo

MOSCOW,URUSI

KIONGOZI  wa Korea Kaskazini,  Kim Jong Un amewasili hapa jana tayari kwa mkutano wake wa kwanza na Rais wa nchi hii, Vladimir Putin leo.

Rais Kim Jong amefikia katika mji wa bandari wa Vladivostok, ambao kwa mujibu wa Kremlin mkutano huo utakaozungumzia masuala ya usalama katika rasi ya Korea hasa tatizo la nyuklia utafanyika.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema Rais Kim kwa sasa anatafuta washirika wapya, baada ya mazungumzo yake na Rais wa Marekani Donald Trump kutibuka.

Wawili hao walikutana mara mbili ya mwisho ikiwa mjini Hanoi, Vietnam mapema mwaka huu kujadili mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Hata hivyo, mkutano huo uliisha bila viongozi hao kufikia mwafaka.

Kiongozi wa Korea Kaskazini ameripotiwa kusafiri kwa treni yake binafsi na kutelemkia katika mji wa mpakani wa Khasan.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kuwasili alisalimiana na wanawake wa Urusi waliokuwa wamevamilia nguo za kitamaduni kuashiria sherehe ya mapokezi yake.

Mwandishi wa Shirika la Utangazji la Uingereza (BBC), Laura Bicker anasema mkutano huu unachukuliwa na wengi kama fursa ya Korea Kaskazini kuonesha washirika wake wakuu baada ya mazungumzo yake ya nyuklia na Marekani kuvunjika.

Mwandishi hiyo anasema taifa hilo linamlaumu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo kwa kuchangia kuvunjika kwa mkutano huo wa Februari mwaka huu.

Mapema mwezi huu Korea Kaskazini ilitaka, Pompeo aondolewe kwenye mazungumzo ya nyuklia, ikimlaumu kuzungumzia upuuzi na hivyo kuomba mtu makini zaidi kuchukua nafasi yake.

Wadadisi wa mambo wanaamini mkutano huu utatoa fursa nzuri kwa Urusi kuonesha ushawishi wake katika rasi ya Korea kutokana na kwamba Rais Putin amekuwa akisubiri kwa hamu kukutana na Kim kwa muda mrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles