22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

RAIS PUTIN APELEKA ASKARI MPAKANI KOREA KASKAZINI

MOSCOW, URUSI


RAIS wa Urusi, Vladimir Putin anatuma askari na silaha mpakani mwa nchi yake na Korea Kaskazini kutokana na hofu kuwa Marekani inajiandaa kumshambulia Rais Kim Jong-un.

Putin anahofu kwamba kutakuwa na wimbi kubwa la wakimbizi kutoka Korea Kaskazini iwapo kiongozi mwenzake wa Marekani, Donald Trump ataanzisha shambulizi la kijeshi.

Hatua hiyo inakuja siku chache tu baada ya kubainika China pia imetuma askari 150,000 katika mpaka wa kusini kukabiliana na wimbi la wakimbizi kutoka Korea Kaskazini ambalo Beijing ina wasiwasi watavuka kukimbia iwapo vita itaibuka.

Picha zilizoonekana jana asubuhi zilionesha namna Putin anavyoimarisha mpaka wake wenye urefu wa maili 11 akimimina askari na zana za kivita. 

Picha ya video ilionesha moja kati ya treni tatu zikiwa zimejaa zana za kivita zikielekea mpakani hapo.

Ushahidi mwingine ni nyendo za helikopta za kijeshi mpakani hapo na uwapo wa magari ya kivita.

Kuna wasiwasi kuwa mgogoro ukiibuka, Urusi itakabiliana na janga la kibinadamu kutoka Korea Kaskazini.

Lakini Putin pia ameonya iwapo Marekani itapiga maeneo ya nyuklia ya Kim Jong-un, mgogoro utafika hadi Urusi.

Juzi Urusi ilizuia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani jaribio la karibuni la kurusha kombora la Pyongyang huku China mshirika wa Korea Kaskazini ikiunga mkono taarifa ya Marekani kulaani tukio hilo.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Lu Kang alisema inachounga mkono ni mpango wowote wa kusitisha uundaji wa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.

Aidha inaunga mkono mpango wa kuimarisha amani na uthabiti katika rais hiyo na kuendelea kutatua masuala tofauti kupitia mazungumzo na majadiliano.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles