21.1 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Rais Nyusi: Kimbunga kimeua watu 1,000

MAPUTO, MSUMBIJI

RAIS Filipe Nyusi amesema idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na kimbunga Idai nchini hapa huenda ikawa ya juu na kufikia 1,000.

Nyusi alisafiri kwa ndege katika maeneo yaliyoathirika zaidi siku ya Jumatatu na akasema kuwa aliona miili ikielea juu ya mito.

Kwa mujibu wa Shirika la Save the Children, tayari kuna hatari ya maisha kwa zaidi ya watoto 100,000 na watu wazima kufuatia kimbunga hicho, huku mito katika maeneo yaliyothirika zaidi ikivunja kingo zake.

Mafuriko yaliyotokea mapema mwezi huu yamezidishwa na kimbunga Idai, ambacho kilikumba eneo la kaskazini mwa nchi na kusababisha uharibifu mkubwa wa nyumba, shule, hospitali na miundombinu.

Kwa mujibu wa Serikali ,takriban watu 600,000 wameathiriwa, huku 100,000 wakihitaji msaada wa dharura mjini Beira.

Wakati hali ikiwa hivyo nchini hapa, katika taifa la Zimbabwe waliokufa kutokana na mafuriko yaliyotokana na kimbunga hicho wanakaribia 100.

Mamlaka ya Zimbabwe imesema Rais Emmerson Mnangagwa alirudi nyumbani mapema kutoka katika ziara ya Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) ili kuhakikisha anashiriki moja kwa moja katika janga hilo la kitaifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,592FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles