23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Rais Mwinyi apokea vifaa vya ujenzi kutoka NMB

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya kuezekea katika kituo cha afya Jang’ombe ili kusaidia ujenzi wa kituo hicho.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, DK. Hussein Ali Mwinyi, wakati wa ziara ya kutembelea kituoni hapo.

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Donatus Richard alisema benki hiyo, imetenga asilimia moja kurejesha kwa jamii  ili kusaidia jamii inayaowazunguka katika mambo mbali mbali.

Alisema wameamua kutoa msaada huo baada ya kupokea changamoto hiyo,na kugushwa na shida ya wananchi  ili kusaidia jamii na kuungana na serikali katika kuleta maendeleao.

Vifaa walivyotoa ni mabati 255, mbao 220 na kilo 100 za misumari kwa ajili ya kuezekea kituo cha afya Jang’ombe ambacho pia hutoa huduma za mama na watoto.

Alisema ndani ya miaka miwili benki hiyo imetumia shilingi milioni 195 kutoa misaada mbali mbali, ikiwemo vituo vya afya na skuli.

Aidha alisema NMB itaendelea kuwa bega kwa bega na wananchi kwa kutoa misaada  mbali mbali ambayo itasaidia jamii inayowazunguka,ambapo pia aliwataka wananchi kuendelea kujiunga na benki hiyo.

Akipokea vifaa hivyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliipongeza benki hiyo kwa kutoa msaada huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles