23 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Mwinyi amezitaka TAKUKURU, ZAECA kuongeza ushirikiano

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amezisihi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kuongeza ushirikiano katika ufanisi wa kazi zao.

Dk. Mwinyi alitoa nasaha hizo Ikulu, Zanzibar, leo Agosti 27,2024 alipozungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila, aliyefika kujitambulisha kufuatia uteuzi wake uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, hivi karibuni.

Rais Dk. Mwinyi amezishauri taasisi hizo mbili kuzidisha ushirikiano hasa kwenye miradi ya kimkakati ya maendeleo kwa maslahi ya Taifa.

Naye Chalamila amemuahidi Rais Dk. Mwinyi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya ZAECA na TAKUKURU katika kufanikisha majukumu ya taasisi hizo.

Amesifu na kupongeza juhudi za maendeleo makubwa zilizofikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dk. Mwinyi.

Amesema, mbali na majukumu mengine waliyonayo, TAKUKURU na ZAECA imekuwa rahisi kwao kushirikiana, hasa katika kudhibiti wahalifu wa pande mbili za Muungano wanaojaribu kukimbilia mipaka ya Bara na Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles