25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS MUSEVENI AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI UGANDA

Na Waandishi Wetu-DAR ES SALAAM


RAIS   Yoweri Museveni wa Uganda ametoa amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kwenda kuwekeza  Uganda.

Kauli hiyo aliitoa   Dar es Salaam jana, alipotembelea viwanda vya Kampuni ya  Bakhresa vya unga na juisi  vilivyopo Buguruni na Vingunguti.

“Ninapenda kuwakaribisha wafanyabiashara wa Tanzania kuja  Uganda kuwekeza kwani kufanya hivyo kutasaidia kuzalisha bidhaa, upatikanaji wa soko pamoja na ajira,” alisema Museveni.

Alitoa kauli hiyo kutokana na mafanikio ya mwekezaji  Said Salim Bakhresa aliyewekeza  kiwanda cha  ngano nchini humo.

  Mkurugenzi wa  Uhusiano wa Kampuni za Bakhresa,  Hussein Sufiani alisema kampuni hiyo iko mbioni kuongeza utoaji ngano kutoka tani 1,100 hadi kufikia tani 2,000 kwa siku nchini Uganda.

Alisema kutokana na uwekezaji wa kampuni hiyo  Uganda,   Waganda 650 wamenufaika na ajira mbalimbali ambazo zinasaidia kuwapatia kipato.

 Naye  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwaijage alisema  Uganda na Tanzania zimeingia makubaliano  ya ushirikiano katika sekta mbalimbali  ikiwamo   ya viwanda.

Alisisitiza Watanzania wanaweza kwenda kuwekeza  Uganda kwa vile nchi hiyo inalima tani milioni nne za mahindi lakini ina uwezo wa kutumia tani milioni moja pekee, hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kwenda kuwekeza nchini humo.

“Tunawahamasisha wafanyabiashara wa Uganda na Tanzania kuwekeza katika nchi zao   kuzalisha, bidhaa na ajira za kutosha kwa wananchi,” alisema Mwijage.

Vilevile, aliwataka Watanzania kushiriki katika uchumi wa viwanda kwa kuzalisha bidhaa zinazotumika viwandani,  mfano kwa kulima matunda au mbogamboga.

Rais Yoweri Museveni aliwasili nchini juzi kwa ziara ya  serikali ya siku mbili ambako   alifanya mazungumzo na Mwenyeji wake Rais Dk. John Magufuli na jana alitembelea viwanda hivyo vya Bakhresa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles