23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

Rais Mugabe awatupia lawama mahakimu Zimbabwe

RAIS Robert Mugabe wa Zimbabwe
RAIS Robert Mugabe wa Zimbabwe

HARARE, ZIMBABWE

RAIS Robert Mugabe wa Zimbabwe, amewalaumu mahakimu wanaoruhusu maandamano dhidi ya serikali, ambayo baadae hugeuka vurugu.

Alisema mahakimu wanadharau amani, na akawaonya kutothubutu kuonesha dharau wanapofikia uamuzi.

Kauli yake hiyo inakuja huku wafuasi wa upinzani leo wakitarajia kwenda mahakamani, kupinga amri iliyopiga marufuku maandamano kwa wiki mbili.

Kiongozi wa upinzani, Tendai Biti, amemshutumu Rais Mugabe kwa kujaribu kuwatisha majaji.

Maandamano kadhaa yaliyoambatana na ghasia yamefanyika nchini Zimbabwe katika wiki za hivi karibuni kuupinga utawala wa Mugabe.

Waandamanaji hao wanataka kiongozi huyo ang’oke huku wakimlaumu kwa ukosefu wa ajira na msukosuko wa uchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles