RAIS MAGUFULI AWATAKA WAKUU WA WILAYA WAMALIZE MIGOGORO YA ARDHI

0
1201

Na Anna Potinus – Dar es Salaam,


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amewataka wakuu wa wilaya mkoa wa Mara wahakikishe wanamaliza migogoro ya ardhi inayotokea katika maeneo yao.

Rais Magufuli alisema endapo watashindwa kufanya hivyo hawatakuwa na sababu ya kutawala wakati watu wan chi moja wanagombea mipaka ndani ya nchi yao.

Rai hiyo imelowewa leo na Rais Magufuli wakati alipokuwa akizindua barabara ya makutano Natta Mugumu wilaya ya Butiama Mkoani Mara, yenye urefu wa kilometa 135 na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara Uwanja wa Mwenge.

“Msigombane, msisubiri viongozi wa nchi waje wawatatulie migogoro yenu, ninawaomba sana msiniaibishe huu mkoa ambao baba wa taifa amelala hapa, pia tusiliingize taifa katika migororo. Na viongozi wa mkoa wa Mara kwa nini mnaacha wananchi wagombanie ardhi wakati kuna maeneo makubwa au mnataka mpeleke wawekezaji?” alihoji

Aidha Rais Magufuli amewataka wananchi wa Butiama wamtangaze na wamuenzi baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuishi kwake kwa upendo na ushirikiano ili Tanzania ifike mbali.

“Ninaomba muendelee kushirikiana na kuwa wamoja, msibaguane kwa sababu ya dini na makabila badala yake tuendelee kumuishi baba wa taifa kwa matendo yake ya upendo na heshima,” alieleza.

Barabara aliyozindua Rais Magufuli leo imegharimu zaidi ya bilioni 54.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here