Na ANNA POTINUS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amewataka maaskofu na mashekhe nchini kuendeleza maombi kwa ajili ya amani ya nchi kwa kuwa ndiyo inayokuza uchumi wa nchi.
Rais amesema hay oleo kwenye uzinduzi wa ujenzi wa daraja la mto Sibiti na barabara unganishi ya mkoa wa Singida na Simiyu.
“Maaskofu na mashekhe mna jukumu kubwa la kuiweka Tanzania kwenye mikono ya Mungu kwani maombi yenu yanasikika zaidi yetu wenye dhambi hasa mimi,” alisema
“Ninawaomba kila mmoja wetu awe muhubiri wa amani kwani tunaihitaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu, leo kungekuwa na vita hata huyu mkandarasi angeshindwa kujenga hili daraja,
Aidha amemjia juu mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa daraja hilo na kumtaka ahakikishe daraja hilo linakamilika haraka iwezekanavyo kwakua pesa zinazotumika ni za wananchi.
“Mkandarasi amesema mvua ndiyo zilizokwamisha daraja kumalizika kwa wakati, wananchi wanahitaji daraja na sio sababu, kwani alipokuwa anaomba kazi hakujua kama hapa maji yanapita? Tusitafute visingizio,” alisema.
Daraja hilo lina urefu wa mita 72 na kilomita za urefu 25, kampuni inayosimamia ujenzi huo ni ya nchini China.