29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Rais Magufuli amjulia hali Sumaye

su2Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli, jana amemtembelea na kumpa pole Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, ambaye amelazwa katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam.

Sumaye amelazwa katika taasisi hiyo siku nne zilizopita kwa matibabu ya moyo na madaktari wanaomtibu wamemhakikishia Rais Magufuli kuwa anaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofikishwa katika taasisi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Gerson Msingwa, ilieleza kuwa pamoja na kumpa pole, Rais Magufuli pia amemwombea kwa Mwenyezi Mungu apone haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kila siku.

Akizungumza mara baada ya kuonana na Rais, Waziri Mkuu mstaafu Sumaye amemshukuru Rais Magufuli kwa kwenda kumwona na kueleza kuwa kitendo hicho kimeonesha jinsi alivyo na upendo wa dhati na anavyowajali watu wake.

Kuhusu hali yake, Sumaye ambaye mwaka jana alitoka CCM na kujiunga na upinzani, alisema anaendelea vizuri, anapata matibabu mazuri na kwamba kwa kuwa hali yake ni nzuri anatarajia kuruhusiwa kuondoka hospitali hapo baada ya muda mfupi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles