22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

RAIS MAGUFULI AIPANDISHA HADHI DODOMA KUWA JIJI

Mwandishi Wetu, Dodoma

Rais John Magufuli, ameupandisha hadhi Mkoa wa Dodoma kuwa Jiji kuanzia leo Aprili 26 huku akisisitiza azma yake ya kuhamia jijini humo iko pale pale.

Uamuzi huo ameutangaza wakati akihutubia kwenye sherehe za maadhimisho miaka 54 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

“Napenda kuwahakikishia Watanzania hasa wa Dodoma kuwa azma ya serikali kuhamia Dodoma iko pale pale na mimi kama nilivyoahidi mwaka huu nahamia Dodoma.

“Lakini pia kuanzia leo kwa mamlaka mliyonipa Watanzania Dodoma ni Jiji na Mkurugenzi aliyekuwa Mkurugenzi wa Manisapaa sasa anakuwa Mkurugezni wa jiji,” amesema Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, amesema Dodoma iko katikati ya Tanzania ambapo sasa ile miradi iliyoombwa na serikali kwa Benki ya Maendeleo Afrika (ADB), wajue haiendi manispaa bali inaenda kwenye jiji.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles