31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Magufuli aiomba China kuifutia madeni Tanzania

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli ameshuhudia Utilianaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka huku akiomba China kusamehe madeni yake kwa Tanzania likiwemo deni walilolibeba wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA.

Akizungumza leo Ijumaa Januari 8, mara baada ya kushuhudia utilianaji saini huo, Rais Magufuli amesema huu ni wakati wa Tanzania na China kujenga uchumi kwa nguvu zote pamoja na kuimarisha ushirikiano.

“Waziri Wang Yi ametuletea ujumbe wa Rais wa China, Xi Jinping kwa sisi Watanzania na hii ni kutokana na mahusiano kati ya Tanzania na China, tumeupokea na mimi nimetuma salamu zangu kwake, tumemuomba kusamehewa deni la takribani dola milioni 167.

“Nimemuomba Rais wa China, Xi Jinping kutufutia deni miliono 15.7 tulilolibeba wakati wa ujenzi wa Tazara , lakini pia deni la dola milioni 137 la nyumba za askari, katika deni hili tumelipa dola za marekani milioni 164.

“Pia tumeomba tusamehewe deni la kiwanda cha Urafiki dola milioni 15, tumewaomba kwa sababu China ni marafiki wetu na nchi tajiri. Tunajua kwa sheria za China kutoa msamaha ni ngumu lakini tumeoma ili waangalie namna ya kutusaidia,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema huu ni wakati muafaka kwa Tanzania kuimarisha uchumi wake kupitia China.

“Ndiyo sababu nimewapa zawadi ya korosho, majani ya chai na kahawa kwani kama China yenye watu bilioni 1.5 wakitumia nusu kilo ya korosho ina maana watahitaji tani milioni 750,” amesema.

Aidha, kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje ya China, Wang Yi amesema amefurahia kushuhudia utiaji saini wa ujenzi wa reli ya kisasa, nakusema kuwa wanategemea jitihada anazofanya Rais Magufuli katika uboresha na kujengwa miundombinu zitaleta maendeleo kama ilivyo kwenye nchi yao.

Wang ameondoka leo kuelekea Visiwa vya Seychelles ambapo ziara yake nchini, inatokana mazungumzo kwa njia ya simu kati ya Rais Magufuli na Rais Xi, Desemba 15 mwaka jana. Hii ni mara ya pili kwa Wang kufika Tanzania na mara ya kwanza ilikuwa Januari 2017.

Ikumbukwe kuwa pamoja na ushirikiano uliopo kwenye sekta nyingine ikiwemo sekta ya miundombinu, uhusiano baina ya Tanzania na China umezidi kuimarika zaidi katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). 

Kupitia kampuni ya Huawei, China imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika kufanikishamiradi mbalimbali inayolenga kuboresha sekta ya TEHAMA sambamba  na kukuza na kuibua vipaji vya sekta hiyomuhimu hapa nchini.

Matunda yaushirikiano huo yalijidhihirisha hivi karibuni ambapo Waziri Mkuu KassimMajaliwa alikabidhi  tuzo kwa washindi washindano la TEHAMA duniani lililoandaliwa na kampuni ya Huawei ambapo wanafunzikutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walishika nafasi ya pili Ulimwenguni.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Mbona nchi yetu ni tajiri? Halafu tunaomba tusamehewe madeni? Kulikoni?
    Hata hivyo kufutiwa madeni kunaambatana na masharti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles