Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameelezea dhamira yake ya kusaidia kukomesha vitendo vya kigaidi na mauaji katika ukanda wa Sahel, Afrika Kaskazini.
Alikuwa akizungumza katika mkutano wa masuala ya Usalama nchini Mali uliohudhuriwa pia na viongozi kutoka nchi tano za eneo hilo, Mali, Mauritania, Niger, Burkina Faso na Chad.
Viongozi hao kwa pamoja wametaka kuungwa mkono, kwa kikosi cha wanajeshi elfu tano wanaopambana na wapiganaji wenye itikadi kali katika ukanda huo wa Sahel.
Rais Macron amesema majaribio hayo ya kupambana na ugaidi yanahitaji juhudi za pamoja kuimarisha maendeleo katika kanda hiyo, ikiwemo mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia ya nchi na kuimarisha utawala bora.