27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Kikwete apiga kura kijijini kwake

jkNA PATRICIA KIMELEMETA, CHALINZE

RAIS Jakaya Kikwete jana alipiga kura kijijini kwake Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Rais Kikwete ambaye anamaliza muda wake wa uongozi wa miaka 10 tangu alipoingia madarakani Novemba 2005, aliwasili kijijini hapo katika Kituo cha Zahanati ya Msoga, jana saa 12:25 na kupanga foleni ya kupiga kura kama ilivyo kwa wananchi wengine.

Baada ya kumaliza kupiga kura, alisema amejitokeza kutumia haki yake ya msingi ya kuwapigia kura viongozi wanaotarajiwa kuongoza katika kipindi kingine cha miaka mitano.

“Matokeo yatatangazwa baada ya kukamilika kwa zoezi ka kuhesabu kura ili ifikapo Novemba 5 mwaka huu, tuweze kumwapisha rais mpya.

“Kwa hiyo, mimi baada ya kustaafu nitarudi kijijini kwangu kwa ajili ya kujiendeleza na shughuli za kilimo na mifugo, kwani mimi ni mkulima na mfugaji,” alisema.

Pamoja na hayo, alisema baada ya kustaafu, ataanzisisha taasisi ya maendeleo ambayo itafanya kazi katika nchi mbalimbali za Afrika na duniani kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, taasisi hiyo itajishughulisha na shughuli za maendeleo ambayo itasaidiana na serikali katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Naye Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM), alisema jimboni kwake upigaji kura ulifanyika vizuri.

Katika baadhi ya vituo, alisema kulikuwa na changamoto ndogondogo zilizojitokeza, ikiwa ni pamoja na baadhi ya watu katika kituo cha Miono kutoona majina yao, licha ya kuwa na vitambulisho vya kupigia kura.

Kutokana na hali hiyo, alisema alitarajia kuendelea kupitia vituo mbalimbali vilivyopo jimboni humo ili kuangalia maendeleo ya zoezi la upigaji kura.

Naye Mgombea Ubunge, jimbo hilo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mathayo Torongey, alisema amepita kwenye vituo vingi kwa ajili ya kukagua zoezi zima la upigaji kura, lakini hajaona tatizo lolote.

Alisema licha ya kuwepo kwa utulivu katika vituo vingi, baadhi ya mawakala kwenye vituo vya Kata ya Msoga wamejiondoa baada ya kutishiwa maisha.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, alisema hadi mchana kulikuwa hakuna tatizo lililoripotiwa, licha ya kuwa baadhi ya maeneo watu walikuwa na hofu kwamba zoezi litakwenda taratibu, lakini hali hiyo iliondoka na utaratibu kwenda vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles