23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS KENYATTA ATANGAZA MAOMBI YA WIKI NZIMA

NAIROBI, KENYA


RAIS Uhuru Kenyatta amewataka wananchi wote kushiriki maombi maalum kwa wiki moja kuliombea taifa wakati uchaguzi mkuu unapowadia.

Rais aliwataka Wakristo na Waislamu, na wananchi wote wa dini zote kuombea amani, utangamano, umoja na mvua.

Alisema hayo juzi wakati wa kuzinduliwa rasmi kwa hamasisho la Kwaresima, ambayo ni imani ya Kanisa Katoliki  kwenye Uwanja wa Michezo wa Chuo Kikuu cha Nairobi.

Mada ya kampeni hiyo ni kuhusu uchaguzi wa amani na unaoweza kuaminika pamoja na viongozi waadilifu.

Aliwaomba kilele cha maombi hayo ifanywe na Waislamu misikitini siku ya Ijumaa, na Wakristo kuungana nao siku za Jumamosi na Jumapili.

“Tuungane sisi sote, tutoe matamshi ya amani nyumbani, kazini na kuwakosoa wote wanaochochea fujo, ninaahidi kutekeleza wajibu wangu kuhakikisha kuwa amani inadumu katika taifa hili,” alisema.

Wito wake umetokea wakati, ambapo kampeni za kisiasa zimezidi kupamba moto na wanasiasa wengi wanashambuliana kwa maneno yanayoweza kusababisha mgawanyiko kwa misingi ya kikabila na kisiasa.

Wakati wa hafla hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya waumini wa Kikatoliki na viongozi wa kanisa hilo, Katibu Mkuu wa Chama cha ODM, Dk. Agnes Zani ambaye aliwakilisha upinzani alieleza utayari wa vyama vyao kudumisha amani wakati wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.

“Tunatazamia uchaguzi wa haki na unaoweza kuaminika na inafaa tuchague viongozi waadilifu. Tulipata mafunzo awali lakini demokrasia haiwezi kuwa bila haki,” alisema Zani.

Wakati wa mahubiri, Askofu Cornelius Korir wa Jimbo la Eldoret aliangazia baadhi ya masuala yanayokabili taifa hili.

Aliwataka wananchi si tu kuomba bali kupigia kura viongozi waadilifu ambao hawawatenganishi wapiga kura kwa misingi ya kisiasa, kikabila.

Aidha Askofu Korir alilaani vitendo vya ufisadi unaotishia kuangamiza maendeleo katika maeneo ya kaunti na taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles