Kigali, Rwanda
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, yuko mbioni kuongeza utawala wake wa miaka 24 kwa miaka mingine mitano katika ushindi wa kishindo, huku kura nyingi zikihesabiwa kutoka katika uchaguzi uliofanyika jana Jumatatu.
Ana asilimia 99.15 ya kura kufikia sasa, na takribani asilimia 79 ya kura zimehesabiwa, matokeo ya awali yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi yanaonesha.
Kagame mwenye umri wa miaka 66 kwa mara nyingine tena hakukabiliwa na upinzani wowote mkubwa, huku viongozi hao wakipigwa marufuku.
Wapinzani wake wawili waligawana chini ya 1% ya kura zilizopigwa. Kagame aliwashukuru Wanyarwanda kwa imani yao katika hotuba katika makao makuu ya chama chake cha Rwandan Patriotic Front (RPF).
“Hizi si takwimu tu, hata ikiwa ni 100%, hizi sio nambari tu. Wao wanaonesha kuamini, na hilo ndilo lililo muhimu zaidi,” amesema Kagame.
Wapinzani wake, Mwanamazingira, Frank Habineza na mwandishi wa habari na mwandishi Philippe Mpayimana, wana 0.53% na 0.32% mtawalia.
Matokeo kamili yanatarajiwa kufikia Julai 20 na ya mwisho ifikapo Julai 27.