27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Kagame aishutumu Burundi kushambulia DRC

 KIGALI, RWANDA

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame amevishutumu vikosi vya Burundi kuendesha mapigano mashariki mawa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), huku akipinga madai kuwa wanajeshi wa Rwanda wako katika eneo hilo pia.

Jimbo la Kivu Kusini huko DRC linakabiliwa na mzozo wa kivita kwa sasa baina ya makundi mengi ya eneo hilo pamoja na waasi wa Burundi na Rwanda wanaopinga Serikali za Bujumbura au Kigali.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Rais wa Rwanda, Paul Kagame alisema majeshi ya Burundi ndio yako katika eneo hilo la Kivu Kusini.

Maelfu kwa maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na mapigano makali ya kijeshi yanayoendelea ambayo yamechacha katika siku za hivi karibuni

Wakazi na baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO’s) yanadai majeshi ya Rwanda na ya Burundi yanapigana sambamba na makundi ya wanamgambo katika mizozo inayoendelea.

Katika mkutano kwa njia ya video na waandishi wa habari Jumatatu, Kagame aliwaambia waandishi wa habari kuwa baadhi ya mashirika yasiyokua ya kiserikali na wataalamu hawaangalii kile kinachoendelea pale, bali wanataka kuona uwepo wa wanajeshi wa Rwanda.

 “Intelijensia yetu inatuambia kwamba tunavikosi kutoka Burundi,vikosi vya serikali, vinavyoendesha harakati zake katika jimbo lile. Hakuna mwanajeshi hata mmoja wa Kikosi cha Ulinzi cha Rwanda (Rwandan Defense Force) ambaye amekwenda katika eneo lile na wanajeshi wa DRC na serikali ya DRC wanafahamu ukweli kwamba hakuna askari wa RDF aliyeko pale,” alisema Kagame.

Alisema kuwa Wanyarwanda walioko huko ni wapiganaji wanaoipinga serikali ya Rwanda wa kundli la FDLR na makundi mengine yanayounga mkono wapiganaji hao.

Kagame alisema jambo zuri kwa sasa ni kwamba Serikali ya sasa ya DRC inakubali kushirikiana na nchi jirani katika kutatua tatizo la miaka mingi la wapiganaji wa msituni.

Oktoba mwaka jana wanajeshi DRC walianza harakati za kuyamaliza makundi yenye silaha katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo, licha ya kwamba harakati hizo hazionekani kuzaa matunda.

Akijibu kuhusu shutuma za Rais wa Rwanda, Mmsemaji wa Rais wa Burundi, Jean Claude Karerwa alikana uwepo wa wanajeshi wa Burundi Mashariki mwa DRC.

Katika ujumbe wake alioutuma kwa BBC, Karerwa alisema: “Labda iombwe na AU au Umoja wa Mataifa, vinginevyo Burundi haiwezi kupeleka wanajeshi wake katika taifa jingine “.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles