26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Rais Donald Trump aendelea kupata nafuu

 WASHINGTON, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump “anaendelea vizuri” baada ya kuwa hospitali kwa usiku mmoja akiwa anaendelea kupata matibabu ya virusi vya ugonjwa wa corona.

Daktari wake binafsi, Sean Conley amesema hapokei matibabu ya oksijeni na pia ndani ya kipindi cha saa 24, homa imeonesha kuisha.

Dk. Conley aliashiria matumaini makubwa kwa afya ya rais lakini akaongeza kwamba hawezi kusema ni lini ataruhusiwa kutoka hospitali.

Rais Trump mwenye umri wa miaka 74, ambaye ni mwanaume na aliye kwenye kundi la wenye uzito kupita kiasi, yuko miongoni mwa walio kwenye hatari ya juu ya kupata ugonjwa huo.

Hadi kufikia sasa amekuwa akipata matibabu ya sindani na tiba ya kuzuia virusi ya remdesivir.

Mke wake, Melania Trump, ambaye pia amethibitishwa kuapata maambukizi ya ugonjwa huo “anaendelea vizuri”,.

Orodha ya watu wengine ambao wamethibitishwa kupata maambukizi walio karibu na Trump ni pamoja na msaidizi wake, Hope Hicks – anayeaminika kuwa wa kwanza kuonesha dalili – mkuu wa timu ya kampeni, Bill Stepien na aliyekuwa mshauri wa Ikulu Kellyanne Conway. Maseneta wa Republican Mike Lee na Thom Tillis pia nao wamesemakana kupata maambukizi.

Mapema Rais Trump alipelekwa hospitali akiwa na homa baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Ikulu ya Marekani ilisema Rais alikuwa mchovu lakini hali yake iko sawa na alipelekwa hospitali ya jeshi la taifa ya Walter Reed kama hatua ya kuchukua tahadhari.

Alipelekwa hospitali chini ya saa 24 baada ya kuthibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Akiwa amevaa barakoa na suti, Rais Trump alitembea hatua kidogo tu katika Ikulu ya Marekani hadi kwenye helikopta yake, akipelekwa hospitali.

Alinyoosha mkono na kuonesha ishara ya kuwa sawa kwa wanahabari lakini hakusema lolote kabla ya kuingia ndani ya ndege.

Katika video iliyowekwa kwenye mtandao wa Twitter, Bwana Trump alisema: “Nataka kumshukuru kila mmoja kwa kuwa nami. Ninaenda hospitali ya Walter Reed. Nafikiri naendelea vizuri.

“Lakini tutahakikisha kwamba mambo yanakwenda sawa. Mke wangu pia anaendelea vizuri. Kwahiyo asanteni sana, nawashukuru, Siwezi kusahau – asanteni.”

Watoto wa rais, Ivanka na Eric, walituma tena ujumbe wa baba yao, huku wakimsifu kuwa “shujaa”. Mtoto wa Trump aliongeza: “Nakupenda sana baba.” Akiwasili hospitali ya Walter Reed, Rais hakupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi, lakini alikwenda moja kwa moja katika sehemu iliyotengwa ya rais, kulingana na kituo mshirika wa BBC Marekani, CBS News.

Mwandishi wa habari wa Rais, Kayleigh McEnany alisema kwenye taarifa: “Rais Trump yuko katika hali nzuri, ana dalili za wastani, na amekuwa akifanyakazi kwa siku nzima.

“Akiwa hayuko katika hatari na kulingana na daktari wake na wataalamu wa tiba, rais atakuwa akifanya kazi katika hospitali ya Walter Reed kwa siku chache zijazo.

“Rais Trump anatoa shukrani zake kwa ujumbe anaopokea wa kumtakia uponaji wa haraka na mke wake.”

Dalili alizonazo Bwana Trump ni pamoja na kiwango cha chini cha joto, kulingana na CBS. Walter Reed, ni hospitali iliyopo viugani mwa Washington DC. Moja ya hospitali maarufu za kijeshi ambapo marais hutibiwa na pia hufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu wa kila mwaka.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu ya Marekani, Alyssa Farah alisema bado hajahamisha madaraka yake hadi kwa Makamu wa Rais,Mike Pence.

Alijiondoa kwenye mkutano uliofanyika kwa njia ya video uliohusisha waandamizi muhimu Ijumaa na kumuacha Pence kuwa mwenyekiti wa mkutano huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles