25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS COMORO AMTUNUKU NISHANI BALOZI KILUMANGA

Na MWANDISHI WETU-COMORO

BALOZI wa Tanzania ndani ya Muungano wa Visiwa vya Comoro, Chabaka Kilumanga, ametunukiwa Nishani ya Juu (Highest Civilian Honor) na Rais wa nchi hiyo, Azali Assoumani.

Kilumanga aliyeongozana na mkewe Irene Kilumanga, alitunukiwa tuzo hiyo juzi katika hafla iliyofanyika Bait Salam, Ikulu ya Comoro.

Wageni mbalimbali walihudhuria hafla hiyo wakiwamo Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Baccar Dossar na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Comoro, Yousef Mohamed Yousef.

Kilumanga anakuwa ndiye balozi wa kwanza kutunukiwa medani hiyo miongoni mwa mabalozi wenzake wanaowakilisha nchi zao visiwani humo.

Wakati akimtunuku medani hiyo, Rais Assoumani, alieleza kutambua mchango mkubwa ulioonyeshwa na Kilumanga katika kudumisha uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na visiwa hivyo pamoja na kumpongeza kwa utumishi uliotukuka.

Kwa upande wake, Kilumanga, alisema amefarijika kutunukiwa tuzo hiyo aliyoshtukizwa na kwamba hiyo ni heshima kubwa kwake.

“Kutunukiwa nishani hii ya kiwango cha juu ni heshima kubwa kwangu na Tanzania kwa ujumla, napongeza juhudi za Serikali ya Rais Assoumani kwa hatua inazochukua katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Comoro,” alisema Kilumanga.

Pia alipendekeza Serikali ya Comoro kuanza kufanya taratibu za kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupanua wigo wa ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles