25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 19, 2022

RAIS BUHARI AREJEA UINGEREZA KWA MATIBABU

RAIS wa Nigeria Muhammadu Buhari

 

 

ABUJA, NIGERIA

RAIS wa Nigeria Muhammadu Buhari amerejea London, Uingereza kwa ajili ya matibabu, ikiwa ni wiki chache baada ya kukaa nchini humo kwa miezi miwili.

Taarifa kutoka Ikulu imesema Buhari anahitajika kwenda Uingereza kuchunguzwa na madaktari.

Hata hivyo, kufikia sasa hakuna taarifa kuhusu ugonjwa unaomsumbua wala muda ambao anatarajiwa kukaa nchini Uingereza.

Anarudi Uingereza akiwa amekutana na wasichana 82 wa Chibok waliokuwa wameachiwa huru baada ya kuzuiliwa na wanamgambo wa Boko Haram kwa miaka mitatu.

Lakini kutokana na afya yake, tukio hilo la kuwapokea juzi halikufanywa kuwa sherehe kubwa.

Buhari amekuwa haonekani hadharani kipindi kirefu cha mwaka huu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
175,234FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles