31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Brazil azuiwa kuingia uwanjani

Rio, Brazil

RAIS wa Brazil, Jair Bolsonaro, jana alishindwa kuingia uwanjani kutazama mechi ya Ligi Kuu nchini humo kati ya Santos na Gremio baada ya kuzuiwa kwa kuwa hajapata chanjo ya Corona.

Iko wazi duniani kote kuwa Bolsonaro amekuwa mstari wa mbele kupinga chanjo ya ugonjwa huo akisema hana imani nazo na mwili wake uko vizuri hata bila ya kuchanjwa.

Hivi karibuni, alilazimika kula ‘pizza’ yake akiwa kando ya barabara na hiyo ni baada ya kuzuiwa kuingia kwenye mgahawa jijini New York, Marekani, ambako kuchanjwa ni kipaumbele katika kupata huduma.

Akizungumza baada ya kuzuiwa kuingia uwanjani, kiongozi huyo amesema: “Kwanini niwe na hati ya chanjo (ya COVID-19)? Nilitaka kutazama mechi ya Santos lakini nikaambiwa nichanje. Kwanini iwe hivyo?”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles