Rais Brazil ahukumiwa miaka 12 jela

0
1054

BRASILIA, BRAZIL

RAIS wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa mashitaka ya rushwa na utakatishaji fedha.

Jaji Babriela Hardt amesema amekubaliana na waendesha mashitaka kuwa nyumba moja ilifanyiwa ukarabati kwa ajili ya Da Silva na kampuni za ujenzi zinazohusika katika ufisadi mkubwa kwenye kampuni ya umma ya mafuta ya Petrobas.

Aprili mwaka jana, da Silva pia alianza kutumikia kifungo cha miaka 12 na miezi 11 baada ya kuhukumiwa kwa mashitaka kama hayo yanayohusiana na ukarabati wa nyumba katika ufukwe wa bahari.

Pia imedaiwa matengenezo hayo yaligharamiwa na kampuni za ujenzi zenye kashfa na malengo ya siasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here