24.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 8, 2022

Rais Bouteflika kujiuzulu kabla ya muhula kumalizika

ALGIERS, ALGERIA

RAIS Abdelaziz Bouteflika wa Algeria anatarajia kujiuzulu kabla ya muhula wake kumalizika Aprili 28 mwaka huu, kwa mujibu wa ofisi yake.

Kauli hii imetolewa huku kukiwa na idadi kubwa ya washirika wa kiongozi huyo mgonjwa wanaojitenga naye huku maandamano dhidi yake yakiendelea.

Taarifa iliyotolewa juzi na ofisi ya rais, ilisema Bouteflika ataondoka madarakani kabla ya Aprili 28, 2019 baada ya maamuzi muhimu kufanyika na kwamba atachukua hatua za kuhakikisha taasisi za dola zinaendelea kufanya kazi zake kwenye kipindi cha mpito.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 amekuwa akionekana kwa nadra hadharani tangu mwaka 2013 alipopata maradhi ya kiharusi.

Maandamano ya kumtaka awachie madaraka baada ya miaka 20 ya utawala wake yameungwa mkono sasa na washirika kadhaa wa zamani wa kiongozi huyo, akiwemo mkuu wa majeshi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,235FollowersFollow
549,000SubscribersSubscribe

Latest Articles