26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Bashir: Maandamano ya kunipinga ni halali

KHARTOUM, SUDAN

RAIS wa Sudan Omar al-Bashir amekiri kuwa madai ya waandamanaji wanaoipinga serikali ni halali isipokuwa tu yalifanyika kinyume cha sheria na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Akizungumza katika hotuba yake ya kwanza Bungeni tangu kutangazwa kwa hali ya dharura Februari 22 mwaka huu, Bashir amesema mgogoro wa kiuchumi umeathiri sehemu kubwa ya raia.

Alisema kutokana na hali hiyo, raia walikuwa na haki ya kuandamana kueleza machungu yao.

Lakini aliongeza kuwa tatizo ni namna yalivyoendeshwa, baadhi waliingia mitaani kuelezea matakwa yao ya halali, lakini wengine waliokusanyika walitumia njia haramu kuharibu mali.

Katika siku za mwanzo za maandamano hayo yaliyoanza Desemba 19, ofisi kadhaa na majengo ya chama tawala cha Bashir vilichomwa moto.

Maafisa wanasema watu 31 wameuawa mpaka sasa katika maandamano hayo, huku Shirika la Haki za Binadamu (HRW) likisema idadi ya vifo ni 51.

Bashir mwenye umri wa miaka 75 ambaye aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi mwaka 1989, awali alitangaza hali ya dharura kwa mwaka mmoja lakini bunge liliipunguza hadi miezi sita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles