27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Rais atishia kupinga matokeo ya uchaguzi

ANTANANARIVO, MADAGASCAR

RAIS wa zamani wa Madagascar, Hery Rajaonarimampianina, amedai kuwa chama chake kimegundua kuwepo kwa dosari nyingi za uchaguzi katika uchaguzi uliofanyika wiki hii, matamshi yanayozusha wasiwasi wa kuzuka kwa maandamano na kupingwa kwa matokeo.

Matokeo ya awali kutoka katika baadhi ya vituo yanamuweka Rais Hery katika nafasi ya tatu nyuma ya wagombea wengine, Andry Rajoelina na Marc Ravalamonana, ambao wote waliwahi kuwa viongozi wa taifa hilo kwa nyakati tofauti.

Rais Rajaonarimampianina akizungumza mjini Antananarivo, amesema uchaguzi huo ulikuwa na dosari za kiufundi ikiwemo orodha ya watu waliosajiliwa kimakosa, vitisho na uwepo wa karatasi ambazo tayari zilikuwa zimepigwa kura.

Kwenye taarifa yake kiongozi huyo amesema hawatakubali kuona wananchi wananyang’anywa haki kupitia kura waliyopiga.

Hata hivyo, matamshi ya Rais Rajaonarimampianina yanakinzana na yale ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika waliotoa taarifa za awali kueleza kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na hapakuwa na dosari kubwa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles