24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

“Rais atasaini Sheria ya Mtandao”

sophia simbaNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, amesema kuwa kutokana na hali ya nchi kwa sasa Rais Jakaya Kikwete, atasaini Sheria ya Mtandao.
Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa akizungumza na MTANZANIA, baada ya kuripotiwa na gazeti moja la kila siku (sio MTANZANIA) mwishoni mwa wiki katika usinduzi wa Kitabu cha Chozi la Sitti, ambapo alinukuliwa akisema kuwa Rais Kikwete ameshasaini sheria hiyo.
Akikanusha taarifa hiyo alisema kuna uwezekano amenukuliwa vibaya ila usahihi wa kile alichosema ni kwamba rais ataisaini sheria hiyo kutokana na hali ya usalama wa nchi kwa sasa.
“Nilishosema si kwamba sheria imesainiwa, maana kwa mujibu wa utaratibu wa sheria ni kwamba sheria yoyote rais akishaisaini inapelekwa taarifa kwa Spika wa Bunge ambaye naye huitangaza.
“Kwa hiyo nami katika uzinduzi ule nilisema kama kukazia kauli ya Ikulu kuwa Rais Kikwete ataisani sheria ile kwani imefuata taratibu zote, ikiwemo kujadiliwa bungeni na hatimaye kuridhiwa.
“Hivyo ninawaomba Watanzania, waelewe kuwa hiki ndicho nilichokisema na si vinginevyo,” alisema Sophia.
Waziri huyo alisema pamoja na mitandao ya kijamii kusaidia kuleta maendeleo na kusambaza taarifa kwa muda mfupi, lakini kuna watu wamekuwa wakiitumia vibaya ikiwemo kuchafuana huku anayeathirika akishindwa kuchukua hatua za kisheria.
Pamoja na hatua hiyo wadau wengi wamekuwa wakimshauri Rais Jakaya Kikwete asiisaini sheria hiyo, kwani inaminya na hata kunyonga uhuru wa vyombo vya habari nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles