24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Rais ataja sababu kumteua mwanamke Wizara ya Ulinzi

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

RAIS Samia Suluhu Hassan ametaja sababu ya kumteua Dk. Stergomena Tax kuwa Waziri wa Ulinzi ni kutaka kuvunja mwiko wa kuwa wizara hiyo lazima iongozwe na mwanaume mwenye misuli.

Akizungumza wakati wa kuwaapisha mawaziri wapya aliowateua leo Ikulu, Dodoma, Rais Samia amesema hata mwanamke anaweza kuiongoza vizuri wizara hiyo kwa sababu lengo ni kusimamia Sera na Utawala na si kubeba bunduki.

Amesema  kwenye hotuba yake ya kuwaapisha mawaziri aliyowateua jana na kuongeza kuwa kazi ya Waziri sio kupiga mizinga wala kubeba mabunduki, ni kusimamia sera na utawala wa Wizara. Nikaamua dada yetu Dkt. Stergomena Tax nimepeleke huko.

“Dk. Stergomena nimempeleka huko si tu kwa kuvunja huo mwiko, ni sababu ya upeo wake mkubwa alioupata akiwa SADC. Kwa uzoefu wake hasa kwenye sekta ya ulinzi atatusaidia. Anawajua askari wetu walioko Msumbiji, DRC, mifumo yao, haki zao, atamsaidia vizuri CDF.

“Makamba sio mgeni nenda kafanye kazi, Mbarawa hii sekta unaijua vizuri (Wizara ya Ujenzi), hivyo ni matumaini yangu mtakwenda kufanya vizuri, uteuzi wenu sio kwamba nyie ni wazuri sana kuliko wengine waliokuweko, uzuri wenu utatokana na utekelezaji wa majukumu yenu.

“Ninachotaka kuona ni matokeo, sio kuwaona tu kwenye TV, tupo hapa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi, nendeni mkaanze kwa kasi, pale ambapo wenzenu walipoachia, mkikuta kuna sehemu ya kufanya mabadiliko fanyeni, muende kwa haraka sana, muda hautusubiri, amesema Rais Samia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles