23 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

RAIS ALI BONGO KUREJEA GABON WIKI IJAYO

Na mwandishi wetu

Rais Ali Bongo wa Gabon, ambaye anatibiwa Morocco baada ya kuugua kiharusi miezi mitano iliyopita, atarudi nyumbani mwishoni mwa wiki hii kwa mara ya tatu tangu alipopatwa na matatizo.

Kwa mujibu wa msemaji wa Rais Ike Ngouoni, Rais Bongo ataondoka nchini Morocco kurudi Gabon Jumamosi Machi 23.

“Rais Bongo anafuraha sana kurudi nchini kwake na pia ametoa shukran zake za dhati kwa Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, kwa kuwakaribisha nchini kwake na kuwapatia msaada mkubwa wakati wote alipokuwa akitibiwa,” amesema Ngouoni

Rais Bongo(60), alianza kuugua mnamo Oktoba 24 akiwa kwenye ziara ya kikazi nchini Saudi Arabia k uhudhuria mkutano mkubwa wa kiuchumi nchini humo.

Tangu ameugua, aliwahi kurudi Gabon mara mbili tu na akikaa chini ya masaa 48 kila alipokwenda, ingawa serikali imekuwa ikisisitiza kuwa yuko imara.

Mwishoni mwa Februari, Rais Bongo iliongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri na kujadili mambo kadhaa, ingawa hakuna vyombo vya habari vilivyotangaza tukio hilo.

Hata hivyo, kutokuwepo kwake kwa muda mrefu nchini Gabon kumesababisha wasiwasi juu ya hali ya kisiasa, kulipelekea kundi la wanajeshi nchini Gabon kutangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya Serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi na kutangaza amri ya kutotoka nje, tukio ambalo halikufanikiwa baada ya wanajeshi waaminifu kwa Serikali ya Rais Ali Bongo kufanikiwa kuzima jaribio hilo la mapinduzi ya serikali Januari 7.

Rais Bongo alichukua nafasi baada ya uchaguzi mwaka 2009 ambao ulifuatia kifo cha baba yake, rais wa zamani Omar Bongo, ambaye alianza kazi mwaka 1967 na kuiongoza nchi hiyo ya Afrika magharibi kwa zaidi ya miaka 40.

Familia ya Bongo imetawala taifa hilo kwa miaka 51 iliyopita, na imetuhumiwa kwa kujilimbikizia mali na utajiri mkubwa kutokana na rasilimali za taifa hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,800FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles