28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Rais aahirisha kura ya maoni yenye utata

CONAKRY, GUINEA

Rais wa Guinea ameahirisha kura ya maoni yenye utata iliyokuwa ifanyike jana Jumapili kuhusu kubadilishwa kwa katiba na iwapo itapita huenda ikamruhusu kuwania tena Urais kwa awamu ya tatu.

Rais huyo, Alpha Condé (81), alisema ameamua kuahirisha kidogo kura hiyo kwa sababu upinzani umedai kuwa maofisa wameingilia orodha ya wapiga kura.

Tangazo hilo lilitolewa huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka kuhusu suala la kura hiyo kufanyika kwa haki.

Maandamano yenye ghasia yamekuwa yakishuhudiwa katika miezi ya hivi karibuni kupinga kura hiyo.

Karibia watu 30 wameuawa katika maandamano ambayo yamekuwa yakifanyika tangu Oktoba.

Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), wamesema kwamba hawatatuma waangalizi wao kwa uchaguzi huo.

Inakadiriwa kuwa raia milioni 7.7 waliosajiliwa kupiga kura pia watapiga kura kuchagua wabunge.

Mapema wiki hii, Shirika la Kimataifa la Wazungumzaji wa Kifaransa, lilisema kwamba kuna tatizo la kutambua majina karibia milioni 2.5 katika sajili ya wapiga kura.

Kwa mujibu wa barua iliyotumwa na Rais Condé kwa Ecowas kuhusu kuahirishwa kwa uchaguzi huo, ambayo ilionekana na shirika la habari la

“Huku hakumaanishi kwamba ni kulegeza msimamo au kurudi nyuma. Raia wa Guinea watamchagua wanaempenda kwa uhuru katika kura ya maoni,” alisema Rais Condé katika runinga inayomilikiwa na Serikali Ijumaa jioni.

Muungano wa upinzani uliokuwa unapinga katiba mpya, FNDC, umetoa wito wa kususia kura hiyo ya maoni na kuongeza uwezakano wa wale wanaoiunga mkono kuibuka na ushindi kwa urahisi.

Hata hivyo, kupitisha katiba mpya kutamaanisha kwamba muda ambao Condé ameshatawala kama rais hautahesabika na muhula wake wa pili unamalizika Desemba.

“Utayari wake wa kubadilisha katiba hauna uhusiano wowote na mpango wa yeye kuwania uraisi kwa muhula wa tatu” Amadou Damaro Camara, mbunge wa chama tawala alisema alipozungumza na BBC.

“Cha msingi ni kuhakikisha kwamba katiba mpya inapatikana kwa nchi ya Guinea kwasababu tuliyo nayo sio nzuri ya haja.”

Lakini chama cha Upizani cha FNDC, kinasema kwamba mabadiliko yote hayo yanaweza kufanywa kupitia Bunge.

“Madhumuni ya Rais Alpha Condé ni kutaka kuendelea kuwepo madarakani kinyume na sheria,” Nadia Nahman, msemaji wa chama cha upinzani cha Union of Democratic Forces of Guinea, aliiambia BBC.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles