25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 4, 2022

Contact us: [email protected]

Raila, Kalonzo kupokonywa walinzi

image33NAIROBI, KENYA

VINARA wa muungano wa upinzani wa CORD, Raila Odinga na Kalonzo Musyoka, ni miongoni mwa maofisa wa zamani wa Serikali watakaoathirika na mpango wa kupunguza idadi ya walinzi kwa watu mashuhuri.

Makamu wa Rais wa zamani, Moody Awori na Musalia Mudavadi ambaye ni kiongozi wa Chama cha Amani National Congress (ANC) pia watakumbwa na mpango huo.

Waziri wa Usalama wa Ndani, Joseph Nkaissery alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kuimarisha usalama wa Wakenya wa kawaida, ambapo maofisa 11,000 wanaolinda watu hao watapewa majukumu mapya.

“Tutachukua walinzi zaidi waliopewa watu wengine mashuhuri si tu kwa magavana. Miongoni mwa watakaopokonywa ni wanasiasa wa zamani, mawaziri na yeyote aliyepewa walinzi wengi kupita kiasi,” alisema Nkaissery Jumamosi iliyopita wakati akihutubia wanahabari ofisini kwake Harambee, Nairobi.

“Watu mashuhuri wametengewa maofisa wa polisi 11,000, idadi ambayo ni kubwa wakati huu, ambao taifa linakumbwa na changamoto nyingi za kiusalama,” aliongeza huku akisema jukumu kuu la maofisa wa polisi ni kuimarisha usalama wa wananchi.

Jenerali Nkaissery alisema mchakato huo wa kupunguza idadi ya walinzi wa watu mashuhuri ulianza wiki mbili zilizopita, huku Gavana wa Mombasa, Hassan Joho akiwa wa kwanza kuathirika.

Hatua ya Serikali ya Jubilee ya kuwaondoa maofisa 100 wa usalama waliokuwa wakiwalinda Odinga na Kalonzo imeshutumiwa vikali na wanasiasa wa upinzani waliodai viongozi hao walipaswa kupewa ulinzi wa kutosha ‘kutokana na hadhi yao’.

Hata hivyo, viongozi hao wa upinzani walikubaliana na Serikali kila mmoja abakie na walinzi 12.

Kuhusu Joho, Waziri Nkaisery alisema gavana huyo alikuwa na walinzi 15 kwa sababu ya hali tete ya usalama katika Kaunti ya Mombasa kutokana na shughuli za kundi la haramu la Mombasa Republican Council (MRC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,538FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles