31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

RAILA ATAKA NGAZI TATU ZA UTAWALA KENYA

NAIROBI, KENYA


KIONGOZI wa upinzani nchini hapa, Raila Odinga, amependekeza katiba ifanyiwe mabadiliko ili kubuniwa ngazi tatu za utawala, kama ilivyopendekezwa katika rasimu ya Katiba ya Bomas.

Akizungumza katika Kongamano la Ugatuzi mjini Kakamega, Odinga alisema hatua hiyo itafanikisha ugavi wa sasa wa rasilimali na kufanikisha malengo ya ugatuzi.

Alipendekeza kubuniwa kwa maeneo 14 zaidi ya utawala, huku Serikali 47 za kaunti zikiendelea kudumishwa kama ilivyo sasa.

“Napendekeza kubuniwa kwa maeneo 14 ya utawala ili kuhakikisha kuwa rasilimali zinasambazwa kwa usawa. Maeneo hayo yatasaidiana na Serikali 47 za kaunti katika kufanikisha ugatuzi. Ngazi hizi za utawala zitafanya kazi kwa ushirikiano na Serikali ya kitaifa,” alisema Odinga, aliyebainisha mfumo huo ulipendekezwa katika rasimu ya Bomas.

Baadaye akihutubia wakazi mjini Kakamega, alifichua kuwa walikubaliana na Rais Uhuru Kenyatta ‘kubadilisha mambo’ na hakuna kurudi nyuma.

“Kama Raila na Uhuru wamekubaliana kufanya hivyo nani anayeweza kupinga?” aliuliza Odinga.

Gavana wa Mombasa. Hassan Joho, ambaye alikuwa ameandamana na Odinga mjini Kakamega, alisema ataongoza kampeni kali wakati ukifika wa kubadilisha katiba.

Mmoja wa wapinzani wakubwa wa harakati hizo za kubadili Katiba, ni Naibu Rais William Ruto, ambaye amekuwa akipinga pendekezo la kubadilisha Katiba hasa kubuni nafasi zaidi serikalini.

Ruto ameahidi kupinga hatua hiyo akisema Serikali ya Jubilee kwa sasa imejitolea kutoa huduma kwa wananchi na haina wakati wa kujihusisha na mjadala wa kubadilisha katiba.

Akizungumza wakati wa ufungaji wa mkutano huo wa ugatuzi jana, Ruto alisema kilicho nyuma ya mpango wa Odinga ni kutoa madaraka kwa watu fulani kinyume, na si mkakati wa kusaidia kaunti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles