25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

RAILA AONGOZA KURA MPYA YA MAONI

NAIROBI, KENYA


SAA mbili tu baada ya  taasisi ya utafiti ya Ipsos kutoa matokeo ya kura ya maoni yakionesha uongozi wa Rais, Uhuru Kenyatta, huku mpinzani wake Raila Odinga akijiimarisha, matokeo mengine yamempa uongozi hasimu wake huyo.

Kampuni ya Infotrak Harris ilitoa utafiti wake siku huyo ya Jumapili ukionesha Raila akiongoza kwa asilimia moja mbele ya Kenyatta baada ya kupata asilimia 47 ya kura kutoka asilimia 43 alizokuwa nazo Juni 30 mwaka huu.

Rais Kenyatta alipata 46 zikiwa zimeshuka kutoka asilimia 48.

Katika kipindi cha kati ya utafiti wa mwisho uliofanywa na kampuni hiyo na juzi Jumapili, Odinga ametembelea eneo la magharibi mwa Kenya mara moja ilhali Kenyatta mara mbili.

Mmoja wa maofisa wa taasisi hiyo, Angela Ambitho alisema mchuano huo ni mkali.

Ambitho alisema kuimarika kwa Odinga kunatokana na kufanikiwa kuwafikia wapiga kura, ambao bado walikuwa hawajaamua katika ngome zake na kujiimarisha taratibu katika maeneo ya Kaskazini Mashariki na Rift Valley.

“Raila amepunguza idadi ya wapiga kura wasioamua katika ngome zake, wakati huo huo akijiimarisha maeneo ya Rift Valley na Kaskazini Mashariki,” Ambitho alisema akirejea ongezeko la asilimia nne alizopata Raila.

Magharibi, ambako kunaaminika ni ngome ya Nasa, kuna idadi kubwa ya wapiga kura ambao hawajaamua, kwa mujibu wa Infotrak.

Wakati wastani wa wapiga kura hao eneo hilo ukiwa asilimia 18, kitaifa ni asilimia sita kwa mujibu wa taasisi hiyo.

Kwa upande wa Kenyatta uungwaji mkono katika maeneo hayo mawili yaliyomnufaisha Odinga ni asilimia 15 Kaskazini Mashariki na asilimia 13 magharibi na asilimia sita eneo la Pwani kipindi cha wiki tatu.

Ambitho, alitoa matokeo hayo saa mbili baada ya Ipsos kutoa matokeo ya utafiti iliyoufanya Julai 3-12 ukihusisha watu 2,209.

Ipsos ilionesha Kenyatta anaongoza kwa asilimia 47 na Odinga asilimia 43, matokeo, ambayo Ambitho alisema huenda ni kwa vile yalifanyika mwanzoni mwa Julai ilhali ya Infotrak yalifanyika hadi juzi Jumapili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles