27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Raila aanika mipango ya kumng’oa Kenyatta

 Raila Odinga
Raila Odinga

NAIROBI, KENYA

KIONGOZI wa Muungano wa Mageuzi na Demokrasia (Cord), Raila Odinga, ameanika mipango ya kumng’oa madarakani Rais Uhuru Kenyatta, akisema ushirika wao utakuwa na nguvu kubwa utakapompitisha mgombea wake wa urais.

Kiongozi huyo wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), alisema muungano wao hautagawanyika kama mahasimu wao wa Jubilee wanavyowaambia wafuasi wao.

Akizungumza katika Kaunti ya Kakamega, Raila alisema ana imani vigogo watatu wa muungano wao; Kalonzo Musyoka (Wiper), Moses Wetang’ula (Ford Kenya) na yeye mwenyewe watafikia mwafaka kuhusu mgombea bora na mwenye nguvu zaidi kuwania urais kwa kuungwa mkono na wote.

Alisema vinara wa muungano huo wameshakubaliana kumuunga mkono mmoja wao na wana imani ya kushinda urais.

Raila alihutubia mkutano wa hadhara huko Shanderema katika jimbo la uchaguzi la Shinyalu kabla ya kuelekea Ileho, ambako alihutubia wanafunzi na walimu katika shule ya sekondari Shanderema.

“Ninawaomba wafuasi wetu kujisajili kwa wingi katika daftari la kura na kujiandaa kwa uchaguzi wa mwaka ujao,” alisema.

Kiongozi huyo mkuu wa upinzani, alianza ziara yake ya siku tano katika Jimbo la Kakamega katika harakati za kupata uungwaji mkono magharibi mwa Kenya, tayari kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Ziara yake Kakamega imelenga kuilinda ngome yake hiyo ya magharibi mwa Kenya, ambayo ilimpigia kura kwa wingi katika uchaguzi wa mwaka 2013.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles