32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Raia wa Uganda akamatwa na mihuri feki ya TRA na Taasisi nyingine za Serikali

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia raia wa Uganda(jina linahifadhiwa) kwa tuhuma ya kumiliki mihuri mitatu ya idara tofauti za Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaaliyokuwa akiitumia kugonga kwenye nyaraka za Magari ya mizigo yanayokwenda Uganda kupitia mpaka wa Mtukula. kinyume na sheria

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera, ACP- William Mwampaghale amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa na mihuri ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisi ya Kilimo na ule wa Ofisi ya Mionzi Tanzania Atomic Energy Commission (TEAC) katika eneo la Mutukula.

Amesema jeshi hilo lilipata taarifa ya siri kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na mihuri ya serikali na amekuwa akiitumia katika shughuli zake kwa kugonga kwenye nyaraka mbalimbali kuonyesha kuwa zimeidhinishwa na idara husika ya serikali .

“Katika kutimiza zoezi hilo tumeshirikiana na idara mbalimbali za ulinzi na usalama ambapo tuliandaa mtego na mnamo 1/9/2022 saa 11:30 jioni huko katika kitongoji cha Katebe Kijiji cha Mtukula na kumkamata mtuhumiwa huyo,” amesema ACP-Mwampaghale.

Aidha, Kamanda huyo baada ya mahojiano na mtuhumiwa huyo alikiri kutumia mihuri hiyo na kueleza kuwa amekuwa akiitumia kugonga kwenye nyaraka bandia ambazo huzitumia kuvusha magari mbalimbali ya mizigo kwenda nchini Uganda.

“Katika mahojiano amesema kuwa hadi sasa amefanikiwa kuvusha magari 11 ambayo ni Fuso na Semi Trailers mawili.

“Mpaka sasa tunaendelea na uchunguzi zaidi ili kubaini mtandao wote wa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya uhalifu hususani katika maeneo ya mipaka mkoani Kagera,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles