24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Raia wa Tanzania wapigwa kufuli kutua Kenya

 NAIROBI, KENYA

SERIKALI ya Kenya imefungua anga lake kwa nchi 11 tu huku baadhi ya nchi jirani ikiwemo Tanzania ikiwa haipo kwenye orodha hiyo.

Pamoja na Tanzania, Marekani nayo haimo kwenye orodha hiyo ya raia wake kuingia nchini humo wakati safari za ndege za kimataifa zitakaproanza tena leo.

Wakati Kenya ikifikia uamuzi huo, Marekani kwa upande wake imeruhusu raia wa Tanzania kuingia nchini humo lakini kwa masharti.

Safari za ndege za kimataifa zilikuwa zimepigwa marufuku tangu Machi mwaka huu wakati maambukizi ya virusi vya corona yalipoanza kushuhudiwa nchini humo.

Waziri wa Usafirishaji wa nchini Kenya, James Macharia alizitaja nchi ambazo ndege zake zimeruhusiwa kutua nchini humo kuwa ni pamoja na China, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe, Ethiopia, Switzerland, Uganda, Rwanda, Namibia na Morocco.

Waziri Macharia alisema, nchi hizo zimedhibiti janga la Covid- 19 kwa kiasi cha kuridhisha.

“Hizi ndizo nchi zilizo na idadi ndogo ya maambukizi, maambukizi ambayo hayana madhara sana ama idadi ya maambukizi yapungua kwa kasi katika nchi hizo,” alikaririwa waziri huyo na gazeti moja nchini humo.

Alisema nchi hizo zimepunguza maambukizi ya ugonjwa huo na raia wake wamekuwa wakipata dalili za kawaida za ugonjwa wa mfumo wa upumuaji.

‘’Tutaendelea kuboresha orodha yetu kwa kutegemea na hali ilivyo na mazingira. Hii ni orodha yetu kwa leo tutaipitia tena kesho na siku zinazokuja.’’

‘’Abiria wote watakaowasili kwa ndege za kimataifa wakiwa na hati zinazoonesha kuwa hawana dalili za Covid-19 na wale waliopima saa 96 kabla ya safari hawatakaa karantini,’’ alisema.

Katika orodha hiyo iliyotolewa na Kenya nchi za Afrika mashariki zilizomo ni Rwanda na Uganda tu.

Alisema hatua ya kufunga anga lao itazihusu baadhi ya nchi tu na sio zote.

Macharia ambaye alikuwa akizungumzia kuhusu mwenendo wa maambukizi ya janga la Covid-19 nchini humo alisema pamoja na kufungua anga kwa ndege za kimataifa, hatua hiyo haitakuwa kwa kila mtu. 

“Ni raia wa nchi 11 pekee wa kigeni ndio watakaoruhusiwa kutua Kenya katika viwanja vyake vinne vya kimataifa vilivyopo Nairobi, Mombasa, Eldoret na Kisumu,” alisema.

Julai 27 mwaka huu, Rais Uhuru Kenyatta alitoa kauli ambayo haikuilenga Tanzania moja kwa moja kuwa Kenya haifichi idadi ya watu wenye maambukizi ya Covid-19.

‘’Sisi tuko wazi na tunajua fika kuwa ugonjwa huu upo tofauti na majirani zetu ambao wanauficha ukweli huu,’’ alisema Rais Kenyatta.

Hatua ya Kenya kuzuia mipaka yake hasa kwa nchi ya Tanzania si mara ya kwanza ambapo awali ilishuhudiwa madereva wa magari makubwa wakizuiliwa kuingia katika nchi hiyo kwa kile kilichodaiwa kutoviamini vipimo vya Tanzania.

Wakati Tanzania ikiwa haijaripoti kisa kipya hata kimoja nchini Kenya idadi ya maambukizi inaendelea kuongezeka.

Kwa mujibu wa gazeti la Tanzania Leo la nchini Kenya, jana, visa vipya vya maambukizi vilivyotangazwa vilikuwa 788 na hivyo jumla ya idadi kufikisha 19,913. 

 Wagonjwa 100 pia walithibitishwa 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles