27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Raia wa Msumbuji, Afrika Kusini wasakwa kesi ya kumteka Mo

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

RAIA wanne wa Msumbiji na mmoja wa Afrika Kusini, wametajwa kuhusika kumteka mfanyabiashara Mohammed Dewji, maarufu Mo, na mahakama imetoa hati ya kuwakamata ili kujibu mashtaka.

Washtakiwa hao walitajwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kuomba hati ya kuwakamata.

Wankyo aliwataja washtakiwa wanaosakwa ili kuunganishwa na mshtakiwa Mousa Twaleb (46) kuwa ni raia wa Msumbiji, Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issa Tomo, Zacarious Junior na raia wa Afrika Kusini, Phila Tshabalala.

Washtakiwa hao wanatakiwa kuunganishwa katika shtaka la pili na la tatu.

Shtaka la kwanza linamkabili Twaleb ambaye anadaiwa kujihusisha na genge la uhalifu, kati ya Mei mosi mwaka 2018 na Oktoba mwaka huo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Johannesburg Afrika Kusini.

Inadaiwa shtaka la pili la kujihusisha na genge la uhalifu linawahusu washtakiwa wote wanaosakwa ili wafikishwe mahakamani.

Shtaka la tatu washtakiwa wote wanadaiwa kuteka nyara. Inadaiwa Oktoba 11 mwaka 2018 katika Hoteli ya Colleseum wilayani Kinondoni, Twaleb akiwa pamoja na wenzake walimteka Dewji kwa nia ya kumuhifadhi kwa siri kinyume cha sheria.

Twaleb katika shtaka la nne anadaiwa kutakatisha fedha Sh milioni nane.

Inadaiwa Julai 10 mwaka jana maeneo ya Mbezi Beach alijipatia kiasi hicho cha fedha huku akijua fedha hizo ni mazalia ya genge la uhalifu.

Kesi itatajwa Agosti 6 mwaka huu na mahakama imeshatoa hati washatakiwa hao wengine wakamatwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles