23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Raia wa Ivory Coast wapiga kura

ABIDJAN, IVORY COAST

HATIMAYE raia wa Ivory Coast jana  wameshiriki katika zoezi la kupiga kura. 

Taarifa zaidi zinafahamisha kwamba baadhi ya wafuasi wa upinzani walijaribu kuvuruga uchaguzi huo baada ya kufuata  wito kutoka kwa wagombea wawili wanaompinga rais Alassane Ouattara.

Wagombea hao wawili wa upinzani  uliowataka raia kususia uchaguzi huo ambapo kiongozi huyo anawania muhula wa tatu. 

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters barabara za mji mkuu wa kibiashara Abidjan zilikuwa na kimya bila watu tofauti na wakati mwingine ambapo zilikuwa zinakumbwa na vurugu uchaguzi.

 Ouattara amesema anagombea tena chini ya katiba mpya iliyoidhinishwa mnamo mwaka 2016, na anafanya hivyo kwa sababu mgombea aliyechaguliwa na chama chake alifariki ghafla mnamo mwezi Julai. Kiongozi huyo anatarajiwa kushinda.

Ouattara amegombea akisema ameitikia wito wa wananchi waliotaka awanie urais.

Kinyangan’yiro cha Urais kilichukua mwelekeo mwingine baada ya Waziri Mkuu, Amadou Coulibaly aliyeonekana kuwa chaguo la Ouattara kama mrithi wake kufariki kwa ugonjwa wa moyo Julai, 8 akiwa na umri wa miaka 61. 

Hata hivyo, uamuzi wake wa kujitosa kwenye kinyangan’yiro cha Urais umeuibua tuhuma za ukandamizaji wa demokrasia wakati wa mihula yake miwili uongozini.

Hapo awali, aliwahi kusisitiza kufanyike mabadiliko ya katiba ili kumuwezesha kuwania muhula wa tatu madarakani.

Miongoni mwa wagombea wengine ni pamoja na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu katika utawala wa Gbagbo Pascal Affis, Henri Konan, na waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Marcel Amon Tanoh.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles