27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Raia 19 wa Ethiopia wanaswa Mwanza

Na FATUMA SAID

RAIA 19   wa Ethiopia wamekamatwa polisi  mkoani Mwanza kwa   kuingia nchini kinyume cha  sheria .

 Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, Jumanne Muliro alisema juzi kuwa raia hao walikamatwa  Machi 19, mwaka huu katika mtaa wa Amani Kata ya Butimba Wilaya ya Nyamagana.

Alisema walikamatwa   nyumbani kwa Benedictor Gervas (57) mkazi wa mtaa huo kwenye chumba alichokuwa amepanga mtuhumiwa  Manka Kagulu (21).

Kamanda  aliwataja raia hao kues ni Alemu Ayule, Degefa Tesfaye, Tsededke Tumisdo, Miratu Labebeu, Sirgage Kemela,Temesgen Dekeyo, Zeleke Dascelegn,Tasela Feyis,Takape Ayeke,

Wengine ni  Zamachu Mathewos, Eshatu Mangasha, Salamu Barekato, Makome Abeba, Amaneui Abana,Gaytso Arflca,Kebamo Gathey, Wondemu Xadesu, Nageshe Ayeye na Degefe Abebe.

 “Jeshi la polisi linafanya utaratibu wa kumpata mkalimani  kuweza kubaini sehemu wanayotoka na wanapokwenda.

“Hivyo watuhumiwa hao wanafanyiwa taratibu za kufikishwa idara ya uhamiaji  hatua nyingine za  sheria ziweze kuchukuliwa,”alisema Muliro.

  Kamanda Muliro alisema  pia kuwa polisi wanawashikilia waganga 16 wa kienyeji wanaopiga ramli chonganishi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza.

Alisema miongoni mwao,  sita ni wanaume  na wanawake ni 10 (majina yanahifadhiwa kwa upelelezi) .

 Vilevile, alisema  polisi wamewakamata watuhumiwa sugu nane wanaojihusisha na matukio makubwa ya uhalifu wakiwa katika hatua za awali kwa kupanga njama ya kutenda vitendo vya uhalifu.

Alisema maji ya watu hao yameifadhiwa   kwa  uchunguzi zaidi na watafikishwa mahakamani pale taratibu za  sheria zitakapokamilika.

  Kamanda Muliro ametoa wito kwa wanachi kutoa taarifa mapema  wanapoona vitendo viovu vinafanyika maeneo yao  polisi waweze kufika mapema na kuzuia uhalifu kutendeka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles