24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

RAGE AUNGANA NA ROSTAM

Na SOSTHNENES NYONI

-DAR ES SALAAM

RAIS wa zamani wa Simba,Ismail Rage amemuunga mkono mfanyabiashara bilionea Rostam Aziz, kwakusema Yanga na klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi zinaweza kupata mafanikio kupitia michango ya wanachama wake bila kutegemea ufadhili wa mtu mmoja.

Juzi akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Rostam ambaye ni shabiki wa Yanga alisema: “Kwa maoni yangu, sioni sababu kwamba ni sahihi kwa timu yenye historia ndefu na ya maana kama Yanga kumilikiwa na mtu binafsi.Sioni uhalali wa timu kubwa kama Yanga kuwa na mfadhili, Ufadhili ni mlango wa nyuma wa umiliki

“Timu ya Yanga ni ya wanachama, ina wanachama kwa mamilioni, haiwezekani kwa mtu mmoja kuimiliki.”

Alisema njia sahihi ya kuiendesha Yanga ni kuendelea kuendeshwa na wanachama wake wote kwa kuichangia, udhamini wa kampuni mbalimbali, viingilio na uuzaji wa bidhaa zake, zikiwamo jezi.

Rostam alisema ili Yanga iwe na mfumo endelevu, lazima iendelee kuendeshwa kwa kupitia michango ya wanachama wake, kuweka uwanja sawa ili wadhamini wajitokeze kuidhamini na kuangalia mfumo mzima wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Alisema suala la wanachama kuichangia timu yao si geni kwani hata klabu kubwa Afrika na Ulaya kama Zamalek na Al Ahly za Misri na Real Madrid na Barcelona za Hispania, nazo zinaendeshwa kwa mfumo huo.

Akizungumza jana na MTANZANIA, Rage alisema  kinachozikwamisha klabu za  Simba na Yanga  si mfumo wa wanachama kuwa wamiliki wakuu, bali viongozi wanaopata fursa ya kuziongoza kutokuwa waadilifu.

“Mimi namuunga mkono Rostam anaposema Yanga inapaswa kuendeshwa na kumilikiwa na wanachama wake, yuko sahihi kabisa, Rostam amewaheshimu wanachama na mashabiki wa Yanga 

“Utajiri wa Simba sio majengo ni wanachama na ‘brand’(jina),  wanachama na mashabiki ni mtaji mkubwa sana wa kuendeshea timu, nenda Iringa utawakuta mashabiki wa Simba, Tanzania nzima wapo.

“ Juventus ilirudisha fedha  zote walizomnunua Ronaldo(Christiano) wakati wanamtambulisha, mashabiki walinunua jezi lakini pia waliingia uwanjani kwa viingilio.

“Tatizo  lililoko  si mfumo wa kuendendesha hizi klabu, shida ipo kwa viongozi wanaopewa fursa ya  kuziongoza kukosa uadilifu tu,”alisema Rage na kuongeza.

“Mfumo wa wanachama kuendesha klabu  hauna shida  yoyote, Ujerumani na Hispania wanautumia na mambo yanakwenda  vizuri kabisa.

“Nataka nikwambie miaka mia moja  Azam  haiwezi kufikia mafanikio ya Simba na Yanga licha ya kwamba inamilikiwa na mtu mmoja mwenye hela.

Katika harambee iliyoendeshwa na klabu ya Yanga Jumamosi iliyopita na kupewa jina la ‘Kubwa Kuliko’ , Rostam licha ya kwa wakati huo alikuwa nje ya nje aliahidi kuichangia Sh .milioni 200 na kuahidi kuendelea kushirikiana na uongozi uliopo kuhakikisha inapata mafanikio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles