31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Rado alamba ‘dili’ kukitangaza kinywaji cha Zhimwa

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam



Muigizaji filamu nchini, Simon Mwapagata maarufu Rado, ameteuliwa kuwa balozi wa kinywaji cha Zhimwa Portable Spirit kinachotengenezwa na Kampuni ya Canon General Supplier.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho leo Jumatatu Oktoba Mosi, Rado ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu kwa mshahara wa Sh milioni mbili kwa mwezi amesema kuteuliwa kwake ni njia mojawapo ya kujitangaza na anaishukuru kampuni hiyo kwa kumchagua.

“Napenda kuishukuru kampuni ya Canon kwa kunichagua kuwa balozi wao wa Zhimwa na nimeipokea kwa mikono miwili na naahidi kuwa balozi mzuri naomba kuungwa mkono,” amesema.

Aidha, Rado amesema wasanii wanapochaguliwa kuwa mabalozi ni njia mojawapo ya kujitangaza wao na kazi zao wanazozifanya ambapo pia ameziomba kampuni nyingine zijitangaze kupitia sanaa.

Naye Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Sufian Mjema, amesema wamemchagua Rado kwa sababu ni msanii mwenye kipaji cha pekee hivyo basi atawasaidia kukitangaza kinywaji hicho ambacho ni kipya sokoni

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles