28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Radi yapiga wanafunzi darasani, mmoja afariki

FLORENCE SANAWA – MTWARA

RADI imepiga katika Shule ya Sekondari Mikindani mkoani hapa na kusababisha mwanafunzi mmoja wa kidato cha tatu, Abdul Athmani kufariki na wengine 32 kujeruhiwa.

 Akizungumza na MTANZANIA, Omar Mhidini ambaye ni majeruhi wa tukio hilo, alisema wakati wakiendelea na masomo, walishuhudia mwanga mkali ulioambatana na muungurumo mkali wa radi uliozua taharuki hali iliyowafanya wajifiche chini ya meza. 

Alisema pamoja na kujificha chini ya meza, baada ya muungurumo huo walibaini kuwa mwenzao mmoja alikuwa ameanguka hali iliyowashtua.

“Ninachokumbuka mwalimu wetu wa Jiografia alikuwa anafundisha mada ya ramani, alipokuwa anamalizia akatoa nafasi ya sisi kuuliza maswali, ghafla ukapiga mwanga mkali ulioambatana na muungurumo wa radi tukajificha chini ya meza zetu, lakini kuna mwenzetu mmoja akaanguka chini na akalala chali,” alisema Mhidini.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, akizungumza mara baada ya kutembelea Zahanati ya Mikindani na Hospitali ya Rufaa Ligula kuona hali za majeruhi, alisema amepokea kwa masikitiko tukio hilo huku akiwasihi wazazi na walezi kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki kigumu.

“Tukio hili ni letu wote, wazazi na walezi nawaomba tuwe wavumilivu kwenye kipindi hiki kigumu, tumepoteza kijana wetu mmoja, lakini pia nawashukuru sana waganga wa Hospitali ya Rufaa Ligula na Kituo cha Afya cha Mikindani kwa kutoa huduma nzuri.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,186FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles