R Kent, Seyram Music wafurahia mafanikio ya ‘Akpe’

0
233

Philadelphia, Marekani

Mwimbaji wa Afro Gospel anayeishi Marekani, R Kent, amewashukuru mashabiki kwa mapokezi ya wimbo, Akpe aliomshirikisha Seyram Music kutoka Ghana.

Kent mwenye asili ya Benin ameiambia www.mtanzania.co.tz kuwa ndani ya wimbo huo amemwagia sifa Mungu kwa mambo makuu ambayo ameendelea kuyatenda pamoja na shukurani.

“Nikiwa kama CEO wa lebo ya ADI Records LLC nimeachia wimbo wangu mpya Akpe au Thank You au Asante, naamini huko Afrika nina mashabiki wengi hivyo naomba sapoti yao ili huduma yangu isonge mbele, video inafanya vizuri sana YouTube hilo nashukuru,” amesema Kent.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here